Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limemtia mbaroni mtuhumiwa, Fikiri Charles(30) kwa tuhuma za mauaji ya wanawake sita kwa kuwakata mapanga, huku mwenyewe akikiri kutekeleza mauaji hayo.

Mtuhuimiwa huyo alipohojiwa na polisi alikiri kuhusika na mauaji hayo na kwamba amesema kuwa huwa anakodiwa kufanya mauaji ya wanawake kwa kulipwa sh. 700,000 hadi sh. 800,000.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi (ASP) Alchelaus Mutelemwa, ambapo amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mwandui wilayani kahama alikamatwa akiwa katika harakati za kwenda kutekeleza mauaji ya mwanamke mwingine.

Aidha, ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikiri kufanya mauaji ya wanawake sita kwa madai ya kuwa amerithishwa na baba yake kutekeleza mauaji hayo kutokana na imani za kishirikina

Hata hivyo, Kamanda Mutelemwa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa dhidi ya wahalifu mapema ili waweze kuwadhibiti.

Maandalizi ya tamasha la vyakula vya asili lakamilika
Video: Dkt. Bashiru, Lowassa watoana jasho mdahalo wa Nyerere, Sababu za kutumbuliwa wakuu wa wilaya hadharani