Ukurasa wa Instagram wa aliyekuwa msanii wa Hip Pop nchini, marehemu Golden Jacob maarufu kama Godzilla umedukuliwa na mtu asiyejulikana na kufanywa kuwa ukurasa wa umbea.

Ukurasa huo kwa sasa umepewa jina la  Umbea Queen.

Farid Kubanda msanii wa Hip Pop nchini mwenye jina la umaarufu Fid Q amesikitishwa sana na jambo hilo kwani ni siku tano tu tangu marehemu Godzilla aage dunia mnamo February 16,2019 na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Hivyo Fid Q ametumia ukurasa wake wa istagram na kuibua jambo hilo ambapo ameandika.

”Yaani hatujafikisha hata wiki tangu tumpumzishe ndugu yetu kwenye makazi yake ya milele…Hackers washapita na page ya insta ya ZIZI”. Fid Q.

Aidha mashabiki wa msanii huyo wamesikitishwa sana na kitendo hiko, harakati za kuirudisha akaunti hiyo zinaendela kufanyika.

 

 

Museveni kuitawala Uganda milele
Majaliwa awataka viongozi CCM kutekeleza majukumu yao

Comments

comments