Mtu mmoja aitwaye Musa Ally mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini Mwanza, amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya 3 hadi chini katika jengo la Rocky City Mall.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Disemba 21, majira ya saa 7:00 mchana.

Aidha, Kamanda amesema kuwa katika uchunguzi wa awali marehemu alibainika kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwasababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

“Uchunguzi wa awali tumebaini kuwa kijana huyo alikuwa na msongo wa mawazo ambayo yalisababishwa na kukosa ajira licha ya kuwa na elimu ya juu aliyoipata chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM,” Amesema Bulimba

Hata hivyo, Kamanda pia amesema kuwa wamekuta ujumbe ndani ya mfuko wa marehemu ambao unaeleza kuwa ana Shahada ya Sayansi ya Kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 22, 2018
Wananchi wambana waziri kuchangia gharama za umeme

Comments

comments