Kila ajira inachangamoto yake, japokuwa kila mtu anaweza akachukulia ajira ya mtu mwingine ni rahisi zaidi kuliko ajira yake, lakini ukweli ni kwamba kila ajira inachangaoto zake ambazo zinamfanya mtu yule aichoke au wakati mwingine atamani kubadilisha ajira yake.

Sasa zipo ajira ambazo zinachagiza kwa asilimia kubwa msongo wa mawazo.

Kutokana na matamanio ya wengi kuona fulani kafanikiwa kupitia shughuli anayoifanya kumekuwa na idadi kubwa ya watu kutamani kufanya shughuli hizo pasipokujua changamoto zake.

Tazama hapa ajira kubwa tano zinazoleta msongo wa mawazo zaidi.

  1. Wapiganaji vita

Hawa huwa na msongo wa mawazo kwa asilimia 72.74, na hii ni kutokana na kwamba aendaye vitani kuna mambo matatu la kwanza unusurike, pili upate ulemavu na la mwisho upoteze maisha kabisa, hivyo ni kazi ya uzalendo mkubwa sana kutokana na matokeo yake.

2. Urubani

Ni kazi ambayo hutumia akili nyingi na inahitaji utimamu wa akili wa hali ya juu, Urubani ni masuala ya kihesabu sana tofauti na udereva, kwani endapo hesabu kidogo ikakosewa kuna hati hati ya kupoteza maisha ya abiria wote waliopo kwenye ndege hiyo, ni bahati sana ajali ya ndege isisababishe vifo, ila mara zote huleta maafa makubwa tumeshuhudia viongozi wengi na watu wakubwa wakipoteza maisha papo hapo kwa ajali ya ndege, mfano kifo cha mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe aliyefariki kwa ajali ya ndege, na mfano mwingine wa mtu mkubwa aliyefariki katika ajali ya ndege ni mmiliki wa klabu ya Leicester city, Vichai Srivaddhanaprabha.

3. Uandishi wa habari

Hii ni kutokana na changamoto ya kazi yenyewe unaweza kuona mtu kama Millard Ayo, Inspekta Chimela, Mercy Mbaya, Maulid Kitenge, Fred War wanafanya kazi rahisi ya utangazaji lakini ukweli ni kwamba kazi ya utangazaji ni moja ya kazi zinazoleta msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa sana kwani kupitia kazi hii wapo waliouawa mfano mwandishi Jamal Ahmad Khashoggi aliyeuawa ndani ya ubalozi wa Saudia Arabia nchini Turkey katika mapigano, wapo wanaolindwa na kutishiwa maisha kutokana na kazi zao pia wapo waliofungwa gerezani na wapo waliovamiwa kutokana na kazi ya utangazaji na wapo waliopotea katika mazingira ya kutatanisha na hawajulikani walipo kutokana na kazi hii mfano hapa Tanzania mwandishi kutoka Mwananchi, Azory Gwanda aliyepotea kwa miezi kadhaa sasa.

Wataalamu wa vipimo wamebaini kuwa kazi hii inaleta  aslimia 47.93 ya msongo wa mawazo.

4. Dereva taxi

Kazi hii inaleta msongo wa mawazo kwa kiasi cha asilimia 48.50, utafiti huu ni kwa mujibu wa jarada la Marekani la Forbes ambapo liliangazia changamoto za wateja wanaokadi gari, pia suala la ulevi lugha za kigeni pamoja na uhalifu, na ugumu wa kazi hii ni kwamba inakutaka umbebe mtu ambaye hujui dhamira yake wala wasifu wake ni kazi ya imani sana, vipo visa vingi sana vinavyowatokea madereva ikiwa pamoja na kutekwa, kuibiwa, kujerihiwa vibaya na wengine kuuawa, mfano mzuri madereva waliwabeba magaidi waliofanya shambulio la kigaidi Nairobi katika hoteli ya DusitD2 wametiwa mbaroni wakidaiwa kuhusika na shambulio hilo kwa namna moja au nyingine.

5. Uaskari

Hii kazi inachangamoto ya asilimia 51.64 kwani kuna changamoto kubwa sana katika kusimamia masuala ya ulinzi na usalama kutokana kwamba kila siku kumekuwa na ripoti ya matukio ya uhalifu na askari ndio watu pekee wanategemewa na jamii katika suala zima la ulinzi, mfano mzuri tukio la tajiri Mohammed Dewji kutekwa watu wa kwanza kushukiwa na tuhuma hizo ni maaskari waliokuwa wanalinda eneo hilo mara nyingi inaeleweka kuwa askari huka njama na majambazi na kuruhusu uhalifu ufanyike katika eneo fulani, hivyo ni moja ya kazi inayoleta msongo wa mawazo zaidi kwani eneo fulani lilikikosa amani watu hawa huusika moja kwa moja.

Video: Ndugai amuita Lissu, asema hana kibali cha kukaa nje ya nchi, Wabunge wa CCM wampongeza CAG
Pacquiao ampiga Broner akimnyanyasa ulingoni