Huko India raia mmoja aliyefahamika kwa jina la Pawan Kumar (25) alichukua uamuzi wa kujikata kidole cha mkono mara baada ya kukosea kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaoendelea.

Amesema alitaka kukipigia kura Chama cha Bharatiya Janata (BJP) katika awamu ya pili ya uchaguzi katika Jimbo la Uttar Pradesh lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo.

Na badala ya kuchagua alama ya Tembo ambayo ndiyo inawakilisha chama hicho, Kumar alibonyeza kitufe chenye alama ya ua ambacho kinawakilisha Chama cha Bharatiya Janata.

”Nilikataka kidole changu kwa kosa hili, Kumar alikiambia moja ya chombo cha habari nchini humo. Aliongeza kuwa alikuwa amekasirika sana na kushindwa kuzitawala hisia zake.

Nchini India alama hutumika badala ya maneno (majina ya vyama) ili kuwawezesha hata wale wasioweza kusoma, wapige kura.

Baada ya tukio hilo alipelekwa hospitali hata hivyo aliruhusiwa kurejea nyumbani baada ya matibabu.

Raia milioni 900 wa India wamekidhi vigezo vya kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu, na hivyo kuufanya uchaguzi wa India kuwa mkubwa zaidi duniani.

Uchaguzi huo unafanyika kwa awamu saba, ambapo umeanza Aprili 11 hadi Mei 19, na matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa

Watu 13 wafariki wakiwa kwenye misa ya pasaka
Leo ni leo: Amir Khan kuzichapa na Terrence Crawford