Wakazi wa kijiji cha Nakapyata, wilayani Buyende nchini Uganda, wamefanya sherehe ya kimila ya kuwaoza watoto wawili walio kati ya umri wa mika tisa na sita, katika utamaduni wa kushangaza.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la Daily monitor la nchini Uganda, Mtoto wa kiume ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Buyande.

Watoto hao woliozwa siku ya jumatatu na kupatiwa nyumba ya kuishi na kitanda, baada ya wote kuripotiwa kuwa walizaliwa wakiwa wameota meno mawili.

Imeelezwa kuwa watoto hao wawili walianza kuchumbiana wakati mvulana alipokuwa na miaka mitatu na msichana alipokuwa na umri wa miezi mitatu pekee, hatua hiyo baadaye iliimarisha uhusiano kati ya familia zote mbili huku Delifazi Mulame mzazi wa mvulana akimuita mtoto huyo wa kike kama mke wa mwanangu.

“Mwanangu alizaliwa na meno mawili na mkewe akazaliwa na meno mawili, kuzaliwa kwake kulileta baraka nyingi na jina lake linapaswa kuwaunganisha watu wa makabila ya Baganda na Basonga” bwana Mulame ameeleza.

Kwa upande wa mwalimu wa mtoto wa kiume Barbra Namulesa ambaye ni mwalimu wa nidhamu shuleni hapo amesema kuwa mtoto huyo ana nidhamu na huzungumza kama mzee wa kijiji na pia hutoa ushauri mzuri pale unapo hitajika.

Naye mama mzazi wa mtoto wa kike Mwandi Mutesi ameeleza kuwa mtoto wake amekuwa mtu wa kushangaza tangu alipozaliwa.

“Alianza kuzungumza mara tu baada ya kuzaliwa, wakati nilipokuwa na uchungu wa kujifungua niliambiwa mtoto ni msichana lakini ana meno mawili, karibu nimuangashe” alisema mamayake aliye na watoto saba.

Na kuongeza kuwa hofu yake ilikuwa kumnyonyesha mtoto mwenye meno.

Nchini Uganda, ni makosa kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 kufunga ndoa ama hata kushiriki katika tendo la ngono.

 

LIVE: Rais Magufuli akizindua mradi wa ujenzi njia ya usafirishaji umeme
Vifo vyaongezeka Mafuriko Iran