Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua wiki ya huduma kwa mteja kwa kuwakaribisha wateja wake wote waliongia madukani kwao kwa kukata keki na kuzindua kifurushi maalum cha  Ofa Kabambe kinachodumu kwa siku tatu ikiwa ni ishara yakuwashukuru wateja wote nchini.

Akiongea katika makao makuu ya Airtel meneja wa duka la Airtel, Celine Njunju amesema wanawashukuru wateja na wananchi wote kwa ujumla katika wiki hii ya huduma kwa wateja inayoanza tarehe 2 hadi tarehe 6 mwezi Oktoba duniani kote.

Amesema kuwa kujiunga na Ofa kabambe ya Airtel Money, kwa Tshs 1000 tu, utapata GB 2, Dakika 110 za kupiga mitandao yote na SMS bila ya kikomo, huku ukiwa na uhuru wa kutumia kifurushi hiki ndani ya siku tatu toka pale ulipo nunua.

Naye Mkurugenzi wa kitengo huduma kwa wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alieleza kuwa wiki hii huadhimisha kila wiki ya kwanza ya mwezi oktoba kila mwaka, lakini Airtel kila siku wanazingatia swala muhimu la kutoa huduma kwa wateja wote kwa viwango vinavyotakiwa

“Mwaka huu Airtel tumeipa wiki hii kauli mbiu ‘Building Trust’ tukimaanisha kuendelea kuwajengea wateja wote Imani katika huduma tunazotoa” amesema Lyamba

Amesema wiki hii Airtel itakuwa na matukio mengi maalumu kwa wateja wao, lakini muhimu zaidi wanawakaribisha wote kutembelea katika ofisi za huduma kwa wateja ili waendelee kujipatia huduma bora kama vile kusajili laini mpya, kujipatia simu na vifaaa vya mawasiliano kwa bei nafuu na vitakuwa na ofa kabambe maalum kwa ajili yao.


Video: HATARI!! “Tulivunja shule baada ya kukosa hela, wazazi wangu walinifanyia kitu cha ajabu sana”

 

Watu 50 wauawa kwa risasi kwenye tamasha Marekani
Gari la Lema lachomoka matairi, adai 'watu wasiojulikana’ wamehusika