Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, amezitaka kamati za rufaa kusikiliza vyema kero za watu wenye malalamiko, ikiweno za wagombea waliokatwa majina yao na kuhakikisha wanayarejesha ili na wao waweze kupata haki zao za msingi.

Hayo yamesemwa leo Novemba 5, 2019, wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma na kuwataka wale wote wenye malalamiko na mapingamizi ya zoezi la uchaguzi linaloendelea, kufika katika ofisi husika ili kuepusha migongano ya kimaslahi.

“Kulalamika ni jambo la msingi na kuna nafasi nzuri ikiwemo nafasi ya mapingamizi na kukata rufaa na ndio maana nimewaambia watu wetu wote wa zile kamati za rufaa, zisikilize malalamiko ya watu kwa msingi na hoja na kuyafafanua vizuri, wale wote ambao watakuwa wameonewa  na majina yao yametolewa, lazima warejeshwe na wapate haki yao kama kushindwa waende kushindwa huko” amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo amekemea baadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa, kukataa kusikiliza malalamiko na kuwataka kuacha mara moja tabia hizo na kwamba wanapaswa kusikiliza malalamiko yote yaliyondani ya uwezo wao na kama watashindwa wayapeleke ngazi za juu.

Mwanafunzi kidato cha nne agoma kufanya mtihani wa taifa, "Sijajiandaa"
Yanga yamfungashia virago Zahera mchana kweupe

Comments

comments