Afya ya rais wa zamani wa Kenya, Daniel Rap Moi imetetereka tena baada ya kurudishwa hospitali na kulazwa zikiwa zimepita wiki mbili tu baada ya kutoka.

Rais huyo amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU), katika Hospitali ya Nairobi na kwamujibu wa madaktari wamesema kuwa ni kutokana na maumivu ya kifua na shida katika kupumua.

Wiki mbili zilizopita, aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo alipokuwa amelazwa huku katibu wa chama cha KANU, Nick Salat akisema Moi alienda kwa uchunguzi wa kawaida wa kiafya.

“Alikuwa hospitalini hapo siku kadhaa nyuma na amerudi tu kwa ombi la madaktari wake, yeye ni mzee na uchunguzi wa mara kwa mara kwa watu wa rika lake ni kawaida tu” amesema Salat.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana, Moi aliondoka kwenda Tel Aviv, Israeli kwa uchunguzi wa matibabu akisindikizwa na mwanawe Gideon na Daktari wake, David Silverstein.

Pombe, Sigara vyawaweka vijana hatarini kupata kiharusi
Mkuchika alia na madeni ya Watumishi