Serikali ya Afrika Kusini ijumaa ya leo imetangaza vifo viwili vya kwanza kutokea nchini humo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona huku idadi ya waathiriki ikifikia 1000.

Akitangaza vifo hivyo waziri wa Afya nchini humo, Zweli Mkhize amesema “asubuhi ya leo tunawaamsha watu wa afrika kusini na habari ya huzuni kwani tumepata vifo viwili vya kwanza kutokana na Covid 19”.

Amesema watu hao wawili wamefariki katika eneo la rasi ya Magharibi huku nchi ikiwa anaendelea na mpango wake wa kujiweka karantini kwa siku 21.

Waziri huyo ameahidi kuendelea kutoa taarifa zaidi juu ya waathirika wa virusi hivyo huku akibainisha kuwa idadi iliyoongezeka jana imefikisha wagonjwa 1000.

Takribani watu milioni 57 wa nchi hiyo watatakiwa kukaa ndani kwa muda wa wiki tatu ili kuepusha maambukizi zaidi.

Nchi nyingine zilizoathiriwa sana na kurekodi maambukizi mengi baada ya Afrika Kusini ni Misri yenye maambukizi 495, Algeria – 367, Morocco – 275, Burkina Faso – 152 na Ghana – 132

Dar: Wanandoa mbaroni kwa kukejeli Serikali juu ya Corona
Uganda: Polisi wamewapiga risasi waliotumia usafiri wa Umma