Mara baada ya Msanii maarufu nchini Diamond Platinumz kuachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha Omarion ”African Beuty”, kumekuwa na mambo mengi yanayoendelea mtandaoni yakihusisha uhusiano wa Diamond na Wema Sepetu hasa mara baada ya Wema Sepetu kuweka ua jekundu mtandaoni akidai kuwa ni ishara ya upendo.

katika siku ya kinamama duniani, Diamond Platinum aliandika ujumbe mzito kuonesha upendo alionao kwa mama yake na kumuahidi kuwa kabla ya mwaka huu kuisha atafunga ndoa, ila bado haijafahamika ndoa hiyo atafunga na nani kwani tayari ipo wazi kuwa ameachana na mama watoto wake Zarina Hassan, na kwa sasa haijajulikana anatoka kimapenzi na nani.

Kumekuwa na uzushi mwingi kwenye mitandao wa kijamii, ambapo post mbalimbali za watu wa karibu wa Diamond Platinumz wamekuwa wakipost kuonesha kuna kitu baina ya Wema na Diamond, ambapo bado hakijawekwa wazi.

Kama ilivyo kawaida ya Watanzania kutabiri mambo, wengine wanasema ni kiki ya wimbo wa African Beuty, wengine Diamond anatarajia kufunda ndoa na Wema Sepetu huku wengine wakidai kuwa ni njama zilizopangwa na wanasiasa kufifisha maandamano yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kufuatia wimbo wa African Beauty umeibua mambo mengi sana ambayo yameleta tafsiri nyingi na tofauti tofauti, ambapo kupitia ukurasa wa instagram wa msanii toka Wasafi, Harmonize ameachia picha ya mpenzi wa Moze Iyobo yaani Aunty Ezekiel na Wema Sepetu picha hiyo imesindikizwa na ujumbe huu.

”African Beauties kama tamu Ramba ….kama chungu tema ndo nishasema, na kumalizia kwa kumtaja mchumba wake Sarah.

Huku dada wa Diamond Platinumz, Esma katika ukurasa wake wa instagram ameachia picha yake akiwa na Wema Sepetu na kusiindikiza na ujumbe uliosema ”asante kwa kuja wifi yangu wa milele” na Wema Sepetu amejibu ujumbe huo kwa kuandika ”Karibu, wifi yangu wa milele, unajua navyokupenda”.

Ni maigizo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii, kwa upande wa Diamond Platinumz bado hajafunguka kwa sasa yupo katika harakati za kuitangaza albamu yake ya A boy From Tandale, amesema wakati ukifika ataweka wazi yote yanayoendelea.

 

50 Cent awaka mrembo kuanika kwenye kitabu walichofanya faragha
Kesi ya mke kumuua mtoto wa mwanasiasa nguli yaunguruma