Afisa mmoja wa idara ya usalama wa taifa nchini Kenya (NIC) amekamatwa pamoja na watuhumiwa wengine wawili kwa tuhuma za kupatikana na bunduki na madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi nchini humo, katika msako uliofanywa Jumapili iliyopita jijini Nairobi, watuhumiwa hao walikutwa na bunduki, gramu 40 za bangi, dawa za kulevya aina ya heroin, hati mbili za kusafiria za Somalia pamoja na vitambulisho viwili vya raia wa Kenya, vyote vikimilikiwa kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao wameendelea kushikiliwa na jeshi hilo wakati upelelezi juu ya tuhuma hizo ukiendelea.

Jeshi hilo limeendelea kufanya oparesheni maalum ya kusafisha ambapo wiki iliyopita, lilimtia nguvuni askari mmoja wa jeshi la polisi ambaye anafanya kazi na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, akihusishwa na tukio la utekaji.

Taarifa ya jeshi la polisi imeeleza kuwa afisa huyo, Constable Kelvin Ndosi pamoja na wenzake watatu walimteka Ochieng’ Okelo Jumamosi iliyopita na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao kisha kumpeleka Kayole.

Chanzo: StandardKenya

Manara na wengine 18 waachiwa kwa dhamana sakata la Mo Dewji
Walinzi waeleza kwanini hawakuwa na bunduki wakati Mo Dewji anatekwa