Kijana Steven Kalunga (29), mkazi wa Kalambo mkoani Rukwa amefaariki dunia katika kijiji cha Miangalua wilayani Sumbawanga wakati akiwa katika jaribio la kuiba pikipiki na fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jastin Masejo amesema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 17, saa 2 usiku katika kijiji hicho.

Kamanda Masejo amesema kuwa siku ya tukio hilo Kalunga akiwa na mwenzake walitega waya mgumu barabarani ambapo mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la Joseph Kachingwe alipata ajali na kudondoka kutokana na mtego huo.

Corona Kenya: Aiba fedha benki kwa madai ya kufanyia kazi nyumbani

Baada ya kuumia ndipo Kalunga na mwenzake huyo waliweza kumvamia na kumpora fedha kiasi cha sh. milioni 1.5 pamoja na pikipiki yake yanye namba za usajili MC 617 CCG na kuipanda kisha kukimbia nayo.

Kachingwe alifanikiwa kuinuka na kupiga kelele za kuomba msaada ndipo kundi la watu walipojitokeza kwa lengo la kumsaidia walianza kuwafukuza watuhumiwa na kutokana na kuwa mwendo kasi mkubwa walipata ajali na kuanguka.

“Katika ajili hiyo, Kalunga aliumia vibaya, alipokimbizwa kituo cha Afya Laela alifariki dunia wakati akiendelea kutibiwa huku mtuhumiwa mwingine akifanikiwa kukimbia na fedha hizo walizozipora” ameeleza kamanda Masajo.

Amesema juhudi za kumtafuta mtuhumiwa aliyekimbia bado zinaendelea ili afikishwe mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Mwanajeshi mbaroni kwa kubaka wanafunzi watatu

Mwanamke afungwa minyororo miaka mitatu, abakwa na kuambukizwa HIV
Ujangili wa wanayamapori wadogo kwa kivuli cha kitoweo kukomeshwa

Comments

comments