Katibu wa mawasilino ngome ya vijana wa Chama cha ACT Wazalendo, Karama Kaila ametoa kauli yao juu ya maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika kesho Aprili 9, 2019 yakilitaka bunge kufuta azimio lake na kuweka katika shughuli zake upokeaji wa taarifa ya CAG.

Karama amekiambia chombo cha habari cha Muungwana kwa njia ya simu na kusema kuwa maandamano bado yako palepale  kwani mpaka sasa hawajapata taarifa rasmi ya kuzuiwa maandamano hayo.

”Kauli yetu ni kwamba maandamano yapo palepale kamanda afuate katiba, katiba inatoa uhuru wa watu kuandamana na watu kutoa maoni kwa hiyo yeye afuate katiba, wananchi ni kwamba hatuna taarifa rasmi ya polisi kutoa ulinzi kwenye maandamano kwa hiyo maandamano yapo palepale mpaka tutapopokea taarifa rasmi kutoka kwa OCD ambaye tumemwandikia barua” amesema Karama.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto leo ameongea na vyombo vya habari na kutahadharisha juu ya watakaoshiriki katika maandamano hayo na kusema kuwa watakaondamana watapigwa watachakaa kwani maandamano hayo ni haramu.

”Kuna chama cha ACT Wazalendo kwa kushirikiana na vyama vingine wanataka kufanya maandamono kesho nataka kuwaambia hao wanaotangaza maandamano kwa njia ya mtandao wakiingia barabarani watapigwa watachakaa, sisi tupo tayari muda wote tupo kwenye mazoezi tunafanya kazi kwakweli tunaawasubiri kama wapo, maandamano  hayo haramu na shughuli za bunge ziendelee na wanachi waendelee  kufanya kazi kama kawaida”. Amesema Muroto.

Aidha Katibu wa mawasilino ngome ya vijana wa Chama cha ACT Wazalendo, Karama alipoitisha vyombo vya habari amesema kuwa hawaoni kama wanakosea kufanya maandamano hayo sababu wanafuata taratibu za kisheria.

Mwili wa Nipsey kuagwa rasmi alhamisi
Waziri wa Usalama wa Ndani Marekani ajiuzulu

Comments

comments