Abiria waliokuwama katika meli ya Diamond Princess Japan, iliyoshambuliwa na virusi vya Corona wameanza kuondolewa leo baada ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa wiki mbili mjini Yokohama.

Zoezi la kuwaondoa abiria hao litadumu hadi ijumaa na karibia Abiria 500 wanatarajiwa kuondolewa kwenye meli hiyo kuanzia leo.

Hadi sasa watu walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19 ndani ya China bara imefikia 74 elfu na vifo kupanda hadi watu 2,004 lakini visa vipya vya maambukizi vimepungua ndani ya siku mbili zilizopita.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mripuko huo bado haujadhibitwa na hali ni ya hatari.

Pamoja na kuifungia miji kadhaa, China inakusudia kuahirisha mkutano mkubwa wa kisiasa wa kila mwaka uliopangwa kufanyika mwezi Machi.

SAFA kuomba uenyeji fainali Ligi ya mabingwa, Kombe la Shirikisho
Siku 18 zabadili upepo wa Emre Can

Comments

comments