Kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah amewaita wachezaji saba kwa mara ya kwanza kwenye kikosi chake, ambacho kitaanza kampeni ya kusaka nafasi ya kufuzu fanali za Afrika (AFCON 2021).

Kikosi cha Ghana (The Black Star) kitacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Afrika kusini Novemba 14, na siku nne baadae kitaanza harakati za kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Afrika, kwa kupambana na Sao Tome and Principe.

Miongoni mwa wachezaji wapya walioitwa kwenye kikosi cha The Black Stars ni mlinda mlango wa Azam FC ya Tanzania Razak Abalora, mshambuliaji Torric Jebrin wa TP Mazembe ya DR Congo.

Mzaliwa wa Hispania alieamua kulitumikia taifa la asili ya wazazi wake Mohammed Salisu akitokea klabu ya Real Valladolid, Iddrisu Baba wa Real Mallorca, Shafiu Mumuni wa klabu ya Ashantigold, Mohammed Kudus wa klabu ya FC Nordsjaelland ya Denmark, na Christopher Antwi-Adjei akitokea  klabu ya Paderborn  ya Ujerumani.

Ndugu wawili Andre na Jordan Ayew, Mubarak Wakaso, Richard Ofori, Felix Annan na Andy Yiadom, ambao kwa pamoja walikua sehemu ya kikosi cha Ghana kilichoshiriki AFCON 2019, nao wametajwa na kocha Kwesi Appiah.

kikosi kamili kilichotajwa na kocha Kwesi Appiah kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Makipa: Richard Ofori (Maritzburg FC, South Africa), Felix Annan (Asante Kotoko, Ghana) na Razak Abalora (Azam FC, Tanzania)

Mabeki: Andy Yiadom (Reading, England), Harrison Afful (Columbus Crew, USA), Lumor Agbenyenu (Real Mallorca, Spain), Joseph Aidoo (Celta Vigo, Spain), Kassim Nuhu (Fortuna Dusseldorf, Germany), Nicholas Opoku (Udinese, Italy) na Mohammed Salisu (Real Valladolid, Spain)

Viungo: Samuel Owusu (Al Fahya, Saudi Arabia), Thomas Partey (Atletico Madrid, Spain), Alfred Duncan (Sassuolo, Italy), Mubarak Wakaso (Deportivo Alaves, Spain), Iddrisu Baba (Real Mallorca, Spain), na Christopher Antwi-Adjei (SC Paderborn, Germany)

Washambuliaji: Andre Ayew (Swansea, England), Mohammed Kudus (FC Nordsjaelland, Denmark), Emmanuel Boateng (Dalian Yifang, China), Jordan Ayew (Crystal Palace, England), Torric Jibril (TP Mazembe, DR Congo) na Shafiu Mumuni (Ashantigold).

Wakati huo huo Kocha Appiah ametangaza kikosi chake, huku uongozi wa chama cha soka nchini Ghana (GFA) ukizindua kampeni ya hamasa ya kufuzu AFCON 2021, iliyopewa jina #BringBackTheLove.

Taarifa ya GFA imeeleza kuwa: “Lengo letu ni kuhakikisha kila shabiki wa soka hapa Ghana anakua na mapenzi na kikosi cha timu ya taifa, tunaamini tukifanya hivi kwa kila mmoja, tutafanikisha mipango yetu ya kuhakikisha tunafuzu fainali za Afrika, na kufuta huzuni iliyotufika wakati wa fainali za 2019 zilizofanyika Misri, kwa timu yetu kushindwa kufanya vyema.”

Chama cha soka nchini humo kwa sasa kinaongozwa na Rais Kurt Okraku, ambaye alichaguliwa juma lililopita, akichukua nafasi ya Kwesi Nyantakyi aliyefungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Rais Kurt Okraku ataongoza kamati malum ya hamasa #BringBackTheLove, akishirikiana na wadau wa soka nchini Ghana.

Jafo akiri uwepo dosari uchaguzi serikali za mitaa
Abiria wapika chai kwenye Treni, Lalipuka nakuua 70 Pakistan

Comments

comments