Kiongozi wa kundi la G-Unit, 50 Cent ameuza jumba lake la kifahari kwa $3 milioni na kutumia fedha zote kutoa msaada.

Mtandao WA TMZ umeeleza kuwa chanzo cha karibu na rapa huyo kimewahakikishia kuwa 50 amefanikiwa kuuza jumba hilo na fedha zote ameziweka kwenye taasisi ya G-Unit Foundation kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa mashirika yasiyo ya kibiashara.

Jumba hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 50,000, lina vyumba 21 vya kulala na mabafu/choo 25. Alilinunua kutoka kwa mke wa zamani wa Mike Tyson, Monica Turner mwaka 2003.

Alinunua jumba hilo kwa $ 4.1 milioni na kisha akatumia $6 milioni kwa ajili ya matengenezo. Mwaka 2007 alilithaminisha kwa $18.5 milioni.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, 50 alilalamika akieleza kuwa anatumia $70,000 kila mwezi kwa ajili ya kulitunza jumba hilo lakini halitumii ipasavyo. Imeelezwa kuwa aliwahi kuliweka sokoni akijaribu kulipangisha kwa $100,000 kila mwezi lakini halikupata mteja.

Jumba hilo lina majiko 9, eneo la kuogelea, sehemu ya kutua helicopter, klabu ya usiku, uwanja wa mpira wa kikapu na eneo lenye michezo ya watoto.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Aprili 3, 2019
Pacquiao kupambana na Mayweather kwenye mchezo mwingine, sio ngumi

Comments

comments