Kiongozi wa G –Unit, 50 Cent ametuliza minong’ono ya waliokuwa wanasubiri aanze kuwauzia vitu baada ya kutangaza kufilisika.

Rapa huyo ameonesha bado anazo za kutosha baada ya kuonesha nyumba yake mpya ya kifahari anayomalizia kuijenga iliyopo barani Afrika.

 

Mwezi Julai  mwaka huu, 50 Cent aliamriwa na mahakama kumlipa fidia ya dola milioni 5 mwanamke ambaye alimdhalilisha kwa kuvujisha mkanda wake wa ngono.

Licha ya kuwa Forbes ilimtangaza kuwa na utajiri wa dola milioni 155, rapa huyo aliiambia mahakama kuwa hana kitu na kwamba anakaribia kufilisika. Aliitaka mahakama kutoamini mbwembwe anazopost kwenye mitandao.

Ujerumani Wajiingiza Mashakani FIFA
Ray C Afanikisha Kukirudisha Kiuno Bila Mfupa