Serikali imesema inafanya ukarabati mkubwa wa reli ya kati inayoanzia Dar Es Salaam kwenda mikoa ya Tabora, Kigoma hadi Mwanza ambao itagharimu takribani dola 300 za kimarekani.

Ukarabati huo umeanza mwaka 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2021 na hivyo kurahisisha huduma kwa watumiaji wa usafiri huo wa Treni.

Akiongea na waandishi wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa eneo la Kilosa hadi Itigi naibu waziri  wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema kuwa ukarabati huo mkubwa unaofanywa ili kuweza kusafirisha mizigo kutoka Dar  es Salaam kwenda nchi za jirani kama Uganda na Rwanda.

Amesema kuwa ukarabati huo pia utasaidia  kusafirisha abiria kwenda mikoa ya Kigoma na Tabora kwa siku mbili kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma ambapo itakuwa tofauti na hivi sasa gari treni hutumia siku tatu.

Naibu waziri alitoa wito kwa wananchi na madereva wa magari wanaopita kukatisha reli kuwa makini kwa sababu  ukarabati huo treni itakuwa inakimbia kwa kasi ya kilometa 72 kwa saa.

Naye Mhandisi Uboreshaji wa Reli ya kati kutoka shirika la Reli Tanzania TRC, Edwin Leonard amesema kuwa uboreshaji wa reli hiyo unafanywa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) inatekelezwa katika vipande vinne ambayo ni Dar es Salaam- Ngerengere- Kilosa – Itigi hadi Isaka na Watanzania zaidi ya elfu mbili na wageni miambili na ishirini wamepata ajira.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kitanzania wamesema kuwa kazi hiyo inawasadia kupata kipato cha kuendesha maisha yao.

Ukarabati wa reli hiyo unakwenda sambamba na Ujenzi wa madaraja, uinuaji wa tuta la reli  pia kujenga vituo vya kudumu vya kusimama trein pindi lifanyapo Safari zake.

Video: Wanafiki CCM wakalia kuti kavu, Wanaofanya miamala ya simu, benki kubanwa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 2, 2019